TCU YATOA TAMKO JUU YA MGOGORO WA IMTU.

UFAFANUZI JUU YA UTEKELEZAJI WA TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MGOGORO BAINA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA IMTU WALIOSIMAMISHWA NA UONGOZI WA CHUO HICHO

Kumekuwepo na tafsiri tofauti kuhusiana na tangazo lililotolewa tarehe 03/11/2011 la Tamko la Serikali kuhusu mgogoro uliopo kati ya Wanafunzi wa Chuo cha IMTU waliosimamishwa na Uongozi wa Chuo cha IMTU, hususani utaratibu wa wanafunzi wa IMTU kuhama kwenda vyuo vingine.

Tume ya Vyuo Vikuu inafafanua kwamba utaratibu wa wanafunzi  kuhama ni kama ifuatavyo, kwanza mwanafunzi atatakiwa kuomba katika chuo atakachokipenda, pili mwanafunzi anatakiwa kuhamia kwenye  kozi ambayo inatambulika na Tume,  tatu mwanafunzi  lazima awe na sifa zinazohitajika kwa ajili ya kujiunga na kozi hiyo,  nne IMTU inawajibika kutuma taarifa ya maendeleo ya masomo (academic transcript) ya mwanafunzi husika na taarifa zote zitakazohitajika za  mwanafunzi  kwenda chuo anachohamia,  tano Chuo kitakachompokea mwanafunzi kinatakiwa kuijulisha Tume juu ya mwanafunzi huyo kuwa hapo chuoni.

Kuhusu makubaliano mengine, Tume ya Vyuo Vikuu imekamilisha taratibu za kufanya ukaguzi wa kina wa chuo cha IMTU (Academic Administrative and Admission Audit) na mara ukaguzi huo utapokamilika mapendekezo ya ripoti yatatumika kwa maamuzi kwa mujibu wa taratibu.

Kwa tangazo hili Tume ya Vyuo Vikuu inaomba wazazi na wanafunzi wa IMTU wafuate taratibu zilizotajwa kuhusiana na wale wanafunzi watakaopenda kuhamia vyuo vingine

Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mtendaji

TUME YA VYUO VIKUU

16.11.2011

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s