MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KESHO.

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
(TACAIDS)

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, 2011 KITAIFA NA MIAKA 10 YA TACAIDS KUFANYIKA SHINYANGA, TAREHE 1 DESEMBA 2011

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inawaarifu wadau wote wa kudhibiti UKIMWI nchini kwamba maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kitaifa mwaka huu yatafanyika mjini Shinyanga, tarehe 1 Desemba 2011. Aidha, maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yataambatana na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TACAIDS. Kilele cha
Maadhimisho hayo kitatanguliwa na wiki ya maonyesho ya shughuli za Wadau wa UKIMWI.

KAULI MBIU KUU YA SIKU YA UKIMWI DUNIA 2011 NI: “TANZANIA BILA YA MAAMBUKIZI MAPYA, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI INAWEZEKANA.

Kauli mbiu ya mwaka huu imetafsiriwa kutoka Kauli mbiu ya kimataifa iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Kimataifa linalohusika na mapambano dhidi ya UKIMWI – UNAIDS inayosema: “GETTING TO ZERO: ZERO NEW INFECTIONS, ZERO DISCRIMINATION AND ZERO AIDS RELATED DEATHS” .

Wadau wa UKIMWI wanaweza kutumia kauli mbiu kuu hiyo kwa ajili ya zana za kujitangaza na vyombo vya habari.
Wadau wote wanaombwa kushiriki katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani. Kwa taarifa zaidi wasiliana na TACAIDS.

MWENYEKITI MTENDAJI
TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA (TACAIDS).
S.L.P. 76987
DAR ES SALAAM
Simu: 2122651, 2125651, 2122427
Barua Pepe: ec@tacaids.go.tz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s