ECKENFORDE TANGA WAGOMA KUSHINIKIZA UONGOZI WA CHUO KUTOWARUDISHA MWAKA WENZAO 11 KWA KUKOSA MIKOPO.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Eckenforde cha mkoani Tanga leo wa wamefanya mgomo chuoni hapo wa kuotingia madarasani kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutowarudisha mwaka wanafunzi wenzao 11  baada ya kukosa mikopo  kutoka bodi ya mikopo.

Akizungumza na wanafunzi wenzake chuoni hapo Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho Ndugu Santus Sangatya alisema kwamba “Tumechanga shilingi 100,000 kila mtu ili wenzetu waliofukuzwa wasiondoke lakini uongozi wa chuo umekataa na umetoa barua wenzetu waondoke hapa chuoni, sisi kama viongozi wenu mliotuchagua hatukubali na  hatuingii darasani mpaka hatma ya wenzetu hawa ambao wamelazimishwa warudie mwaka kwa sababu ya mikopo itakapo julikana”.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafuzni Ndugu Santus Sangatya akionyesha barua iliyoandikwa na uongozi wa chuo ya kuwataka wanafunzi 11 kurudia mwaka baada ya kukosa mikopo kutoka bodi.

Makamau wa Rais akisisitiza jambo juu ya msimamo na hatu azilinazoendelea kuchukuliwa katika hatma ya wanafunzi wenzao.

Viongozi wa serikali ya wanafunzi wakiwa kwenye ofisi ya mlezi wa wanafunzi Bw. Zawadiel Mkilindi, ambapo uongozi huo ulienda kutaka kupata maelezo juu ya sababu za hatua ya uongozi wa chuo kutoa barua ya kuwataka wanafunzi 11 kati ya 64 wa shahada ya uwalimu mwaka wa pili kurudia mwaka baada ya kukosa mikopo kutoka bodi ya mikopo.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s