MAHAFALI MZUMBE YAFANYIKA HII LEO: NCHIMBI APATA PhD.

WAZIRI wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi, leo ametunukiwa Shahada ya Uzamivu katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, mkoani Morogoro. Wahitimu wengine ni Gustav Kunkuta, Simon Lushakuzi, Sunday Makama wa Nigeria, George Makoma, Anarabbi Nangawe na Fred Rwechengula. Pembeni ni bibie Stellar Mtei ambae nae alitunukiwa shahada ya kwanza chuoni hapo.

Bi. Stellar Mtei akiwa mwenye furaha kwenye mahafali hayo..Jumla ya wahitimu 1,365 walitunukiwa katika Kampasi Kuu ya Morogoro hii leo,wakati 472 watatunukia shahada za uzamili katika Shule ya Biashara ya Mzumbe ya Dar es Salaam Desemba 16 na 383 watatunukiwa shahada zao kwenye Kampasi ya Mbeya Desemba 10, mwaka huu.

katika wahitimu hao 1,282 ni wanaume na 938 ni wanawake,” mahafali hayo yalitanguliwa na warsha iliyofanyika ljana katika chuo hicho. “Kwa mara ya kwanza katika historia ya chuo hicho wahitimu walitunukiwa shahada ya elimu katika Lugha na Uongozi ( Bachelor Education in Language Management),Shahada ya Elimu katika Biashara na Uhasibu (Bachelor of Education in Commerce and Accounting) na Shahada ya Elimu katika Uchumi na Uongozi (Bachelor of Education in Economics and Management)

 

 

Advertisements

2 responses to “MAHAFALI MZUMBE YAFANYIKA HII LEO: NCHIMBI APATA PhD.

  1. Tunashukuru kwa taarifa, na wahitimu wote watumie elimu yao sasa kuleta maendeleo! Ila mkuu hujatuambia Dr. Nchimbi katunukiwa Shahada ya Uzamivu-PhD ya kitu gani.

  2. congratulations to Hon E. Chimbi kwan jitihada zako zaonekana , congrtlation to miss stella and many others from mzumbe unversity gob be with you,
    BE BLESSED, ELISHA NKWIJA, NAKURU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s