CHUO KIKUU CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI 2010/2011.

Ikiwa imebakia siku moja kabla ya kufanya mahafali ya chuo hicho mwaka huu chuo kikuu cha Ardhi cha jijini Dar es salaam kimetoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mwaka wa masomo 2010/2011 kutoka fani mbali mbali chuoni hapo.

Zoezi hilo lililohudhuriwa na mkuu wa chuo Prof. Idrisa Mshoro kama mgeni rasmi, bodi ya chuo, wawakilishi kutoka vyuo mbalimbali na makampuni mbalimbali limeendeshwa kwa nia ya kuwapa hamasa wanafunzi wa chuoni hapo ambao asilimia kubwa wanachukua fani za sayansi zinazoaminika kuwa na ugumu kwa wanafunzi wengi.

Utaratibu huo wa utoaji wa zawadi unafanyika kila mwaka chuoni hapo ikiwa ni siku moja kabla ya mahafali ya kuhitimu shahada za kwanza, shahada za uzamili ( MSc.) na shahada za uzamivu ( PhD), ambapo  mahafali hayo ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tar 3 mwezi huu siku ya jumamosi chuoni hapo.

Prof. Mshoro akimakabidhi cheti Victor Sofia..Best DEGREE in overall perfomance BSc. LAND MANAGEMENT AND EVALUATION.

Ramadhan Shauri mwanafunzi bora katika somo la Urban Economics anaesoma BSc. In Real Estate Finance and Investment akipokea cheti chake toka kwa Mkuu wa chuo. uku kwa mbali ndugu waandishi wa habari wakichukua tukio hilo. Hongera sana mdau.

Mdau Ramadhani Shauri baada ya kupoke gamba lake toka kwa mkuu wa chuo..hapa alikuwa anawasuburi ndugu waandishi wa habari hawapo pichani wapate kuchukua picha za kumbukumbu.

Uongozi wa Chuo pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali kwa mwaka 2010/2011 mara baada ya sherehe hizo.

Ramadhani Shauri (kushoto) akiwa na mwalimu wake Prof. kironde (Katikati) anaefundisha Urban Economics katika chuo hicho somo ambali Bw. Shauri amekuwa mwanafunzi bora kwa mwaka uliopita) na Alice Makoba.

Mdau Ramadhani Shauri akiwa na mkuu Bi. Ummy Bakari wakipata chakula katika tafrija hiyo.

Advertisements

2 responses to “CHUO KIKUU CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI 2010/2011.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s