KUTOKA SAUT: MDAHALO KUHUSU MIAKA 50 YA UHURU (Tulikotoka, Tuliko na Tuendako) WAFANYIKA LEO HII.

Taasisi ya Jitambue Foundation kwa kushirikiana na Start Tv kupitia kipindi cha Hoja Yangu leo kimefanya mdahalo na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza katika ukumbi wa M1 uliopo chuoni hapo.

Mtoa mada mkuu katika mdahalo huo alikuwa ni Prof. M.E. Mlembeti ambae alianza kwa kueleza kwamba kiongozi ni lazima ajue hali halisi ya nchi na kisha kutengeneza malengo ya kujua nini cha kufanya na kisha kuwa na mikakati na miradi inayoweza kuzalisha maendeleo katika Taifa.

Akianza kumzungumzia Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere, Prof. Mlambiti alisema kuwa ” Baba wa Taifa alijua matatizo ya Taifa ndio maana aliainisha kuwa umasikini, ujinga na maradhi ndio matatizo makuu yanayoisumbua Taifa na kisha akatumia sera za kijamaa na kujitigemea pamoja na azimio la arusha katika kutatua matatizo haya, alitengeneza mikakati maalum kuhakikisha malengo yanafanikiwa kwa kuanzisha sera za ujamaa vijijini na kisha akaweka mikakati ya kufuatilia utekelezaji wa mikakati hiyo”.

Aidha Prof. Mlambiti alisema kuwa ” Mafanikio yetu hapo baadae yanategemea uwajibikaji na utekelezaji wa mikakati tuliyojiwekea” kisha akamalizia kwa kusema kuwa Uhuru na Umasikini haviendani, tunahisi kuwa hatutendewi haki na serikali lakini sisi ndio tulioichagua serikali hiyo iwepo madarakani na kuibadilisha kwake ni kwa kuchagua kiongozi sahihi wa kuiongoza nchi yetu. Pia serikali inatakiwa isiingilie chaguzi zinazofanyika nchini inatakiwa kuwapa watu uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka.

Mtoa mada mkuu katika mdahalo huo Prof. Mlambiti akitoa mada juu ya Miaka 50 ya uhuru kuangalai tulikotoka, tulipo na tunakoenda.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jitambue Foundation ndugu Isaack Mwanahapa akichokoza mada mbele ya wanafanzi wa SAUT hawapo pichani mara baada ya Mtoa mada mkuu kumaliza kuongea.

Mchangiaji wa kwanza katika mdahalo huo Bw. Steven Leberian anaesoma shahada ya Uwalimu mwaka wa tatu, alisema kamba " mtu hawezi kuwa huru kama ni masikini na huwezi kuwa huru kama rasilimali za nchi hazifaidishi wananchi hivyo uhuru anao mtu mwenye mali na anaekula keki ya taifa hili"

Bw. Gerald Lucas mwanafunzi wa mwaka wa pili shahada ya mawasiliano ya umma akitoa mchangowake " Inauma sana pale wanafunzi wa vyuo vikuu wanakosa mikopo lakini viongozi hao wanaokula keki ya taifa walisoma bure, Tanzania inajengwa na wenye moyo na inaliwa na wenye meno".

Gerald Komba mwanafunzi wa shahada ya sheria mwaka wa tatu akitoa mchango wake " Miaka 50 ya uhuru cheo cha Mwalimu nyerere cha uwalimu kinadhalilishwa, miaka 50 ya uhuru wanafunzi wanaopata daraja la tatu la ufaulu ndio wanaojiunga na uwalimu na upolisi, Watanzania tuwe na dira moja ya maendeleo, tuondoe ushabiki wa kisiasa.

Mwalimu Anna kutoka BAED mwaka wa tatu alisema kuwa "Elimu bora haitokani na nchi kuendelea kuwashawishi wanafunzi waliofeli kujiunga na uwalimu, Afya za wananchi ni kitu cha msingi"

Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Mkolani Elias Benedector nae alipata nafasi ya kutoa mawazo yake "anaipongeza serikali kwa kujenga shule za msingi nyingi sana lakini shule zimejengwa bila hata ya kuwa na miundombinu ya kutosha kukidhi mahitaji ya shule hizo kama vyoo, ofisi za walimu pamoja na madawati huku serikali ikibase kwenye misada kutoka nje inafika kipindi watoa misaada wanachoka na kutoa masharti hata ya ushoga"

Mwanafunzi kutoka Mkolani shule ya Sekondari kidato cha tano, alisema kuwa "Vijana ndio chachu ya kuleta maendeleo katika taifa akigusia mifano kutoka kwenye biblia ya jinsi kina Musaa walivyokuwa vijana walioleta mabadiliko katika mataifa yao.

Vodacom Ambassadors wa SAUT nao walikuwepo katika kuonyesha Bidhaa ya WEB BOX kutoka VODACOM kwenye mdahalo huo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s