KUTOKA ARDHI UNIVERSITY: WASICHANA WAONGOZA MASOMO YA SAYANSI.

Wanafunzi wasichana, wameongoza katika orodha ya wanafunzi bora 95 wa fani tofauti za utaalamu wa matumizi ya ardhi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), jijini Dar es Salaam, waliotunukiwa tuzo za kufanya vizuri kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ya masomo chuoni hapo.

Masomo yanayofundishwa na ARU, mengi ni sayansi ya hifadhi ya mazingira, ardhi na majenzi na upimaji, ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakitawaliwa zaidi na wanaume. Mafanikio ya wanafunzi wasichana yalibainishwa jana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Mengiseny Kaseva, wakati wa sherehe ya kutunuku tuzo kwa wanafunzi hao. Profesa Kaseva alisema kati ya wanafunzi waliofanya vizuri katika kipindi hicho chuoni hapo, asilimia 53.7 ni wasichana.

Wote walitunukiwa tuzo hizo na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Professa Idrissa Mshoro katika sherehe hizo jana. Profesa Kaseva alisema asilimia saba ya wanafunzi wasichana waliodahiliwa chuoni hapo, wamepata tuzo ya wanafunzi bora kulinganisha na asilimia 2.3 ya wanafunzi wavulana waliopewa tuzo ya aina hiyo.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa tofauti na fikra iliyozoeleka, wanafunzi wasichana wana uwezo wa kushindana na wanafunzi wavulana katika masomo ya sayansi na uhandisi.

Naye Profesa Mshoro alisema lengo lake ni kutambua mafanikio yaliyofikiwa na vijana hao ili wanafunzi wengine wanaofuata waweze kuiga. Alisema wakati wakitambua mchango huo, wamefurahishwa na juhudi zinazofanywa na wasichana katika taaluma baada ya kuongoza kwa asilimia 53 kati ya wanafunzi wote waliotunukiwa vyeti hivyo.

“Tofauti na miaka ya nyuma, hivi sasa wasichana wamekuwa wakifanya vizuri katika masomo jambo linalotupa faraja na kuashiria safari yao nzuri kitaaluma kadri tunavyozidi kusonga mbele,” alisema Profesa Mshoro.

Sherehe za kuwatunuku wanafunzi bora, zilifanyika kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya Mahafali ya Tano ya ARU, ambazo zinafanyika leo. Zaidi ya wasomi 300 wanategemewa kukabidhiwa shahada mbalimbali katika taaluma ya matumizi ya ardhi, ujenzi, upimaji ardhi na mazingira.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s