KUTOKA SUZA: DK. SHEIN AWATAKA WATENDAJI WA CHUO CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) KUBADILIKA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Wajumbe wa Baraza pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), na kuelekeza haja ya kubadilika katika utendaji wa kazi kwa lengo la kukiendeleza na kukiimarisha zaidi chuo hicho.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na viongozi wa chuo hicho cha Zanzibar katika Kampasi ya Vuga mjini Unguja mara baada ya kutembelea jengo la Taasisi ya Elimu endelevu pamoja na kupata maelezo mafupi ya jengo la majestik.

Katika maelezo yake kwa viongozi hao wa (SUZA), Dk. Shein alieleza kuwa umefika wakati kwa uongozi wa chuo hicho kubadilika ili kuweza kukiimarisha na kukiendeleza zaidi chuo hicho ambacho kinatimiza miaka kumi hivi sasa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein, akizungumza na Bodi pamoja na Uongozi wa Chuo hicho katika ukumbi wa jengo la Makao Makuu ya Chuo hicho Vuga Mjini Zanzibar jana.

Mjumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Simai Mohamed akitoa mchango wake katika mkutano huo kwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Chuo hicho Dk. Shein hayupo pichani.

Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dk. Shein alipotembelea chumba cha kompyuta katika chuo hicho.

Dk.Shein akiagana na viongozi na wajumbe wa Bodi ya Chuo hicho.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s