MAKALA ZA THE MPAGAZE TIMES: MKAKATI WA KUTUUA WALIUANZA ZAMANI, KISA…AFRIKA NI TISHIO KWAO.

Na. Denis Mpagaze, Mhadhiri Msaidizi-SAUT

http://www.mpagazedenis.blogspot.com

Naanza makala yangu hivi, “Our African borther Kanali Muamar Gadafi aliuawa kwa sababu alikuwa katika harakati za mwisho za kuiunganisha Afrika”. Mnamo tarehe 20 Oktoba, saa saba mchana nikiwa darasani nafundisha wanafunzi wangu wa mwaka wa pili katika kozi ya mawasiliano ya umma nilipokea ujumbe kupitia simu yangu ya kiganjani ikisema hivi, “BREAKING NEWS:GADAFI NO MORE”. Na usiku wake vyombo vyote vya habari vya Tanzania vikaanza ushabiki wa kuripoti kifo cha kanali badala ya kutoa uchambuzi pevu wa kifo cha brother huyo. Matamko ya kinafiki kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Kiafrika yalianza kumiminika mithili ya mabomba ya maji yaliyong’olewa koki. Tumepokea kifo cha Gadafi kwa mshituko na masikitiko makubwa. Walikuwa wapi kumsaidia? Wizi Mtupu.
Siyo Botha tu, katika kitabu cha bwana Graham Hancock kiitwacho, “The Lords of Poverty: The Power, Prestige, and Corruption of the International Aid Business” amejaribu kuonesha raisi mmoja wa marekani akifafanua kwamba misaada wanayopeleka katika nchi za Afrika siyo kwa ajili ya kuwasaidia waafrika bali kuwasaidia wamarekani. Mwandishi anasema watoa misaada wamekuwa wakichangisha pesa nyingi na kujinufaisha wao kwa kuchukua pesa kidogo na kununua vyakula vilivyo expire huko kwao na kutuletea afrika ili kutumaliza taratibu. Siri hii sijua kama viongozi wetu wanafahamu maana kila kukicha wanapishana kwenye makorido ya ulaya wakiomba misaada ambayo ni sumu kwa maendeleo yetu. Misaada ni mkakati wa kumuangamiza mtu mweusi. Leo Tanzania imeingia kwenye rekodi ya ulimwengu kuwa nchi ya kwanza kupokea misaada kwa afrika na ya tatu Duniani. Soma Gazeti la Mwananchi Jumatano 7/12 kama unaleta ubishi.

Miaka ya 1930 bwana Jesse Owen (mweusi) alipokuwa wa kwanza katika mashindano ya mbio ndefu kipindi cha Olympic alinyimwa mkono wa pongezi kutoka kwa bwana Hitler Adolf kwamba ni mnyama. Hiwezekani mnyama kushindana na binadamu, lazima tu binadamu atamshinda. Hii ni ishara kabisa watu weusi tuko juu hivyo wanatafuta kila namna ya kuangamiza juhudi zetu.

Na kitu wanachokiogopa sana ni pale tutakapoonesha juhudi za kutaka kuiunganisha Afrika, hapo walahi ukiwa na ideas kama hizo lazima wakuondoe. Kwame Nkrumah yuko wapi? Alipoteza maisha haraka sana pale alipojifanya kuja na idea za kuunganisha Afrika. Unakumbuka katika kikao kimoja huko Addis Ababa Nkwame alipohitilafiana na Nyerere? Nkwame alitaka kuunganisha Afrika, Nyerere akamwambia hapana, tuungane kidogokidogo na baadaye afrika nzima. Mpaka Nyerere anatutoka ile kidogokidogo imeshindikana na hata Zanzibar aliyofanikisha kuunganisha leo inatupa shida. Ukiangalia muungano wa United States of Amerika ulivyokuwa ni siri yao. Ulikuwa wa lazima na leo ni Taifa lenye nguvu. Wao wanadumisha muungano, sisi wanaturubuni kutengana. Unaona kinachotokea Sudan leo? Ni furaha kwao.

Ghadafi aliliona hili na alikuwa katika harakati za mwisho za kuiunganisha Afrika, na kwa uwezo na akili alizokuwa nazo huyu bwana mwakani angefungua benki ya Afrika. Benki hii ingetunasua midomoni mwa IMF na WB zenye masharti magumu ambayo yameua nchi za Kiafrika kabisa. Bila shaka unahabari za Structiral Adjustment Progrma (SAPs). Tangu zimekuja hatujapata kupumua. Soma kitabu hiki How Rich Countries Got Rich … and Why Poor Countries Stay Poor cha bwana Erik Reinet..uone hawa watu wanavyopendana. Sasa walipoona juhudi za Ghadafi zimekwenda kasi wakaamua kumuondoa na viongozi wa Afrika wenye majeshi makali walishindwa kwenda kumsaidia. He who pays for the pipper controls the tune. Wale mnaokwenda kilabuni mnafahamu maana ya msemo huu.

 Kumbe kunahaja ya viongozi wetu kujiongeza
Advertisements

One response to “MAKALA ZA THE MPAGAZE TIMES: MKAKATI WA KUTUUA WALIUANZA ZAMANI, KISA…AFRIKA NI TISHIO KWAO.

 1. Hali ni ya kutisha sana!!
  Misaada yote ni maafa kwa mwafrika.
  Fikiria vyandarua vya bure hivi!!
  Vyenye viatilifu! Siamini kama ni nia njema kwa waafrika.

  UKIMWI pia ni makusudio ya wazungu kuwangamiza waafrika ili kulichukuaBara hili bila tabu!!
  Hali inatisha sio kidogo!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s