KUTOKA ECKENFORDE: WANAFUNZI WATAKA TCU KUKICHUNGUZA CHUO HICHO.

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Eckenforde Tanga wameitaka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuunda Tume ya haraka kuchunguza viwango vya elimu za wahadhiri wa Chuo hicho kwani hadi sasa kuna utata wa kuwepo baadhi ya wahadhiri wasio na sifa za kufundisha ngazi hiyo.

Aidha wanafunzi hao wameitupia lawama TCU kwa kutoa idhini ya kuanza Chuo hicho ilihali hakijatimiza masharti muhimu ya elimu ya juu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wanafunzi hao walisema tangu chuo hicho kianzishwe mwezi Februari mwaka jana hadi sasa hakijaweza kuweka Muongozo unaokielezea chuo hicho yaani.

Walisema kutokuwepo kwa mwongozo huo kunaleta mashaka juu ya uwezo mdogo wa wahadhiri hao katika ufundishaji na hivyo kuzusha hofu ya wanafunzi hao kuweza kuingia katika soko la ajira pindi watakapohitimu masomo yao chuoni hapo.

Akizungumza kwa waandishi wa habari Ofisa Uhusiano wa Taasisi ya Elimu ya Eckenforde inayomiliki Chuo Kikuu hicho, Minihaji Msagati alikiri kuwepo kwa matatizo chuoni hapo na kuwataka waandishi wa habari kukutana naye kutolea ufafanuzi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s