KUTOKA UDOM: WANAFUNZI WA SOSHOLOJIA (UDOMSSO) WAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU KWA SHEREHE YA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA.

Chama cha Wanafunzi wanaosoma masomo ya Ustawi wa Jamii (sociology) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMSSO), usiku wa kuamkia leo kimefanya sherehe za kuwakaribisha mwaka wa kwanza zikiambatana na sherehe za Miaka 50 ya uhuru katika ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma usiku wa kuamkia hii leo.

Sherehe hizo zilizofana sana siku ya jana ambapo zilihudhuriwa na Kaimu mkuu wa  wilaya ya Dodoma Mjini Gerald Guninita ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na  wahadhiri pamoja na wanafunzi. UDOMSSO ni chama chenye malengo ya kuwasaidia wanafunzi kielimu kwa nadharia na kimatendo, kusadia kwa kina kuchambua na kufanya kwa vitendo mwaswala ya sociolojia ndani na nje ya UDOM, Kuongeza taaluma ya sociolojia na kutengeneza daraja kati ya wanachama wanachama wa chama hicho ambacho walengwa wakuu ni wanafunzi wa fani ya ustawi wa jamii katika chuo kikuu cha Dodoma.

Mgeni rasmi ambae ni Kaimu mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Gerald Guninita (wa pili kutoka kulia) akiwa meza kuu pamoja na wahadhri wa Chuo Kikuu cha Dodoma wa shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha Dodoma katika sherehe ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza wa shahada ya sosholojia ya Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika katika ukumbi wa royal village usiku wa kuamkia leo.

TUKATE KEKI PAMOJA: Dada Zainabu Na Kaka Mussa wote kutoka Mwaka Wa Kwanza Wakikata Keki kuashiria Ishara ya Furaha na Upendo Katika Sherehe ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza iliyofanyika Katika Ukumbi Wa Royal Village usiku wa kuamkia leo

Kaimu MKuu Wa Wilaya Ya Dodoma Mjini akilishwa keki na Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Zainabu katika Sherehe ya kuwakaribisha Mwaka Wa Kwanza wa Sosholojia wa UDOM.

Wawakilishi wa Mwaka Wa Kwanza Wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa mbele kuwawakilisha wenzao wa mwaka wa kwanza katika sherehe ya kuwakaribisha iliyofanyika katika ukumbi wa royal village usiku wa kuamkia leo.

Baadhi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiwa na furaha ya sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa shahada ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa royal village.

Mziki ukafunguliwa na mgeni Rasmi..

Twende kushoto shoto sho..twende kulia lia lii....cheza kisauzi sauzi sa...ilikuwa ni wote on stage...hakuna kumuacha mtu.(Habari kwa Hisani ya UDOMSSO BLOG).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s