LEO NI SIKU YA MAADHIMISHO YA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI.

Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu (Desemba 10 2011) -Viwanja vya Mnazi mmoja
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mwaka huu ( 10 Desemba 2011) itafanya maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu katika viwanja vya Mnazi mmoja na Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Mhe.Celina Kombani Waziri wa Katiba na Sheria. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki za binadamu na Mitandao ya kijamii. Wananchi wote mnatangaziwa mfike uwanjani kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja ili kushiriki maadhimisho haya muhimu.Waziri wa Katiba na Sheria. 
Maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu ni moja kati ya jitihada za jumuia ya kimataifa katika kulinda, kuhifadhi, kukuza na kutetea haki za binadamu duniani kote. Tarehe 10 desemba 1948 Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliridhia kutangaza Azimio la kimataifa la Haki za Binadamu(Universal Declaration of Human Rights).
Kutokana na tukio hilo la kihistoria , Mkutano wa Umoja wa Mataifa ulihimiza nchi wanachama kuhakikisha kwamba Azimio hili linatangazwa,linawekwa wazi, linasomwa na kufundishwa mashuleni na katika taasisi za elimu bila kuathiriwa kwa misingi ya itikadi za kisiasa,kidini,jinsia,rangi au maskani ya mtu. katika kuenzi hilo iliamuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa tarehe kumi (10) ya mwezi wa kumi na mbili kila mwaka iwe ni siku ya Haki za Binadamu. Tanzania ilianza kuadhimisha maadhimisho haya kwa mwaka 2008 kwa hiyo hii ni mara ya tatu.
Katika kuelekea kilele cha kuadhimisha siku hiyo Tume imeratibu mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Majaji ishirini na saba wa kanda. 

Bw.Warioba akitoa elimu ya mitandao ya kijamii kwa UN clubs za shule za sekondari pamoja nao ni Vicky Ntetema, Bw. Rioba

Tume pia imetoa mafunzo kwa wanafunzi  wa shule za Sekondari  za Kibasila, Layola na Ruvu Secondary. Mafunzo hayo ni katika kuwawezesha wanafunzi kuweza kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na blogs mbali mbali ili kuweza kuelimishana kuhusu haki za binadamu na pia kuwezesha kuripoti vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wanafunzi wa UN clubs kutoka shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es salaam wakisikiliza kwa makini elimu ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

Sambamba na hayo Tume inategemea kupokea malalamiko na kutoa msaada wa kisheria katika mikoa ya Dodoma(Mpwapwa), Singida (Iramba), Morogoro (Kilosa), Pwani (Bagamoyo) na Mwanza(Geita). kwa upande wa Tanzania visiwani kazi ya kutoa msaada wa kisheria na kusikiliza malalamiko itafanyika Unguja na Pemba.

Tume inatarajia kuwa na Mihadhara ya wazi(Public Lecturer) katika chuo kikuu cha SAUT – Mwanza.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s