RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI JENGO JIPYA LA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais Jakaya Kikwete akikata utepe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mh. Henri De Raincourt kuashiria kufunguliwa rasmi kwa jengo jipya la Chuo cha Taifa cha Utalii jijini Dar es salaam, Kushoto ni Waziri wa Utalii Mh. Ezekiel Maige na kulia ni Mtendaji mkuu wa chuo hicho Bi. Agnes Mziray.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mh. Henri De Raincourt wakizindua plakadi katika sherehe hizo.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mh. Henri De Raincourt wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania Bi. Agnes Mziray mara wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la chuo hicho lililopo mtaa wa Garden Avenue na Shaaban Robert mkabala na Chuo cha IFM na Makumbusho ya Taifa na nyumba ya Utamaduni.

Rais Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa Chuo hicho mara baada ya kuzindua jengo la chuo hicho.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mh. Henri De Raincourt wakioneshwa moja kati ya madarasa yaliyopo katika jengo hilo jipya na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania Bi. Agnes Mziray.

Maktaba kubwa iliyopo katika jengo hilo ambayo itatumika chuoni hapo, Chuo hiki ni maalum kwa kutoa taaluma za maswala ya utalii nchini ili kuweza kuiboresha sekta ya utalii Tanzania hivyo ni moja kati ya hatua nzuri serikali imeifanya.

Majiko ya kisasa kabisa yatakayotumika kama sehemu ya kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Mafunzo kwa vitendo yatafanyika humu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s