HOTUBA YA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO KIKUU CHA MT. AUGUSTINO (SAUTSO), MWANZA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA CHUO KILICHOFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 17/12/2011 KATIKA UKUMBI WA M13 CHUONI SAUT.

Tumsifu yesu kristo, salam aleikum!

Naomba nitumie fursa hii kwa pamoja kuwashukuru kuwepo hapa wakati huu,

Naomba nitumie fursa hii kumshukuru Mola kwa kuendelea kunipa uhai na nguvu kuwaongoza wanafunzi wenzangu.

Nitumie nafasi hii kuwapongeza ninyi wote kwa kufaulu na kuendelea kuwepo chuoni hapa.

Napenda pia nitoe shukrani zangu kwa uongozi wa chuo, mshauri wa wanafujnzi mama Nasania, mwadhini wa wa  chuo  na mwisho si kwa umuhimu, nahamu mkuu wa chuo, kwa ushirikiano wao kwangu, serikali yangu na wanafunzi kwa ujumla.

Ni takribani miezi nane tangu tuingie madarakani serikali yetu ili tuwatumikie wanafunzi wenzetu   kwa kauli mbiu ya “uongozi wenye maono,  malengo na mwelekeo”

Ni kauli mbiu iliyobeba ilani yetu ya uchaguzi kwa wananchi ni ilani iliyoahidi kuwa dira na mwongozo wetu katika kuongoza na kujiongoza.

Ilani yetu ilibeba ajenda zipatazo kumi ,(1) ambazo ni serikali uwakilishi sawa,shirikishi lililo wazi, uwajibikaji, uvumilivu na heshima,yenye , (1)mikopo,(3) taaluma, (4)malazi,(5) ulinzi(6) makundi maalumu(7),Afya, (8)mazingira na chakula(9), michezo na furaha,(10) usafiri na mawasiliano pamoja na  maswala  ya  kijamii.

Serikali yangu ninayoiongoza imejitahidi kuwa serikali ya watu kutoka kwa watu,  na watu kwa ajili ya watu.

Tumewahudumia watu kwa unyenyekevu  kupokea na kutatua kero za watu,  kwa kadri ya uwezo wetu

Tumewajibika kutoa ufafanuzi pale palipohitajika , tumetoa taarifa na maelekezo mbalimbali kwa  wakati, tumekuwa wazi na wasikivu pia.

Swala la mikopo ndiyo injini  na inatafasiliwa kama ndiyo kazi hasa ya serikkali na nikiri hapa zipo changamoto za kutosha hata hivyo tumejitahidi japo katika mazingira magumu kufanya yafuatayo,

Mosi kwa mara ya kwanza tuliwawezesha wanafunzi wa sheria wote kupata pesa ya field,

Pili tumewezesha pesa ya field kutolewa kwa wote pasipo kuzingatia mwaka wa masomo.

Tatu, tumejitahidi sana kutoa taarifa zozote zinazohusu kukawia kwa mkopo, kufika kwa  mkopo,  kusaini mikopo na maelekezo mbali mbali madarasani pale ilipobidi ili kufafanua na kutuliza munkari kwa madarasa ambayo yamekuwa na  changamoto za kimikopo  nimefika utalii , engineer, philosophy na sheria mwaka wanne. tumefanya vikao mbalimbali na maafisa wa bodi ofisini kwangu hata bodi DSM. Inatulazimu  mara nyingine kutumia mbinu ya  robbing and advocacy ili tupate na  kuwahishiwa mikopo na  tumefanikiwa pia.  Pia  tumeweka  timu  ya kutosha yenye upendo, uvumilivu, uwazi  na ukweli na uwajibikaji katika eneo hili, ukifika  utapokelewa  kwa tabasamu na bashasha. Hata hivyo katika hili sehemu kubwa ya changamoto zipo nje ya wigo  wa serikali yetu.

Nne, chuo chetu kwa muda wote wa uongozi wangu kimekuwa cha kwanza kupata mikopo,

Katika taaluma mengi tumefanya na  mengi tunatarajia  kufanya, utakumbuka kuwa muda wa mapumziko hasa kati ya semista  na semsita  haukuwepo, mapema tu baada ya kuingia katika muda mfupi, kwa sasa upo wa wiki mbili  katikati ya semisita na pia siku za kupumzika katika sherehe na matukio ya  kitaifa zipo za kutosha, library na studio  hakukuwa  na jenerator  tulikaa na uongozi zaidi ya mara mbili  tulisisitiza hili tayari jawabu lipo. Tulikaa kikao cha taaluma na makamu mkuu wa chuo DVCAA mnamo tarehe 13/05/2011 na kukubaliana yafuatayo.

Mosi  tatizo la wanafunzi la kitaaluma na lisiwepo kwa zaidi ya wiki.

Pili  tuwe na nidhamu ya masomo tuepuke kuiba mitihani tuwe na uhusiano mzuri na  viongozi wa chuo

Tatu, procurements wapewe fursa ya kufanya workshops zaidi ili kujijengea uwezo zaidi

Nne  report za field zitolewe ili kujua kama kweli field ipi wapi na vipi imefanyika .

Jumamosi nimefanya kikao na DVCAA  na kukubaliana juu ya  wanafujnzi ambao ni wengi na  walikuwa wakifulika hadi nje ya madarasa yao wakati wa vipindi ,tumejadiliana juu ya utata katika provisional result, viti vya kukalia kwa nje kwa ajili ya mijadala na personal study. Viti vilivyokuwa vikikaliwa sasa vitakuwa  released.

Serikali hii imeandaa Academic forums  mbalimbali nyingine kwa ushirikiano na vitivo, tumefanya  mdahalo wa  katiba, tumeandaa nyerere day,  kumefanya  Rwanda,Burundi,Uganda,Kenya, DRC congo. Watoa mada kama VC Dr.  Kitima, Dr Miriam matembe, JE

enerali Ulimwengu, Khalid Mlanga, Aderatus Kilangi, Dr. Safari na mh Lazaro Nyalandu walitoa mada tamu. kongamano kubwa la Africa Mashariki la aina yake katika ukanda.

Kuhusu ulinzi ,uongozi wa chuo  una mtazamo tofauti na serikali yangu wa kuwa na kituo cha polisi, VC alisisitiza ulinzi wa patrol na wa kampuni ya kukodi japo alikiri udhaifu mkubwa uliopo katika kampuni ya ulinzi.

Nasikitika kusema kwamba huduma rafiki kwa watu waalio katika mkundi maalumu bado  uongozi haujalipa uzito wa kutosha hata hivyo  nafurahi kuwataarifu  kuwa upande wa library sehemu maalumu pale chini imetengwa kwa watu hawa kupata huduma.

Kuhusu afya, mazingira  na huduma za chakula tumekaa  na  viongozi kwa ajili ya kuboresha eneo hili, kwanza matabibu wameongezwa pale zahanati ya chuo, madawa yapo, ufasi na  uhakika wa vipimo bado ni changamoto. Katika moja ya safari zangu nje ya nchi nimekutana na  mama mmoja  wa Canada  aitwaye Kay Marris ambaye ni raisi wa Key foundation  ambaye amekubali mwaliko wangu mwezi ujao kuja Tanzania kutoa misaada ya vifaa vya kisasa  katika zahati yetu na  pia kutoa msaada katika kituo  chochote cha watoto yatima kilicho karibu.

Kuhusu chakula kwanza tulifanya  tenda bodi ili kusaili na kupata watoa huduma wapya na mama Mkinga catering, mama Mdamo,  mama Kashekulo na Mr zaharia (quick choice) na Makuli  Seifu(burger) Walipatikana,  wengi wetu ni mashahidi juu ya huduma zinazotolewa na watu hawa wapya achilia mbali gharama zake ambazo ni changamoto ya kimfumo wa bei kitaifa, hata hivo tumejitahidi kuudhibiti.

Pia niliunda timu ya tenda kupata mwekezaji mpya katika eneo la celtel point ambapo  waziri wa sheria na katiba mzee Manyama John  aliongoza timu na flaming catering service Ltd waliibuka washindi,  wanao mpango kabambe wa kupageuza kuwa bora na penye mvuto wa ajabu kutakuwa ka  mali fulani kwa kutoa huduma zote za vinywaji chakula saloon, Atm, maduka  n.k.

Changa moto iliopo sasa ni gharama za chakula bila kutokana maneno wala kuyapindisha ukweli ni kuwa ilikuwa ni vigumu sana watu hawa kuendelea kuuza chakula cha aina yote kwa shilingim 1000 au 1200 hasa kwa kuzingatia hali halisi ya maisha ya sasa nchini, kila  kitu kimepanda.

Serikali yangu, uongozi wa chuo pamoja na watoa huduma ya chakula tulifikia mwafaka kuwa baadhi ya chakula kipande kama kuku wali 1500, samaki wali 1500, mixer 1500 na  vyakula vingine kama wali  nyama , ndizi nyama viwe  1200, wali dagaa, wali magarage  iwe sh 1000 na  tumewaelekeza waweke  wazi hizo bei ili mtu asikose chakula, iwe ni utashi wa mlaji kama atapenda nini.

Kuhusu michezo kwa  furaha  napenda kusema kwamba shughuli mbalii mbali za kiburudani zimefanyanyika kama ifuatavyo:-

Mosi TBL walifanya tamasha lao hapa  na kutoa zawadi mbalimbali

Pili kampuni la Pepsi pia walifanya tamasha lao hapa ambapo mwanamziki   Afande sele alikuwepo katika tukio hili.

Tatu kampuni la zantel  wamefanya  tamasha lao na kutoa zawadi mbali mbali.

Nne,  mashindano ya fawasco yalifanyika kwa ufanithi , ubunifu  na staili mpya, japo zawadi ya VC  ilichelewa kutoka   lakini ile ya SAUTSO  pamoja na kuiboresha pia tuliitoa palepale.

Tano, galla night kawa  mara ya kwanza ilifanyika kwa ufanisi mkubwa ambapo mwanamziki aliyekuwa akishindanishwa kupata tuzo ya  MTV kwa jina la CPwaaa  alitumbuiza kwa kiwango bora kabisa kana kwamba haitoshi  tukio hili liliboreshwa na kuleta mvuto na  shamrashamra nyingi; vinywaji vingi, mziki mzuri chakula  kizuri na kitamu, ninyi ni mashahidi.

Sita, Bonefire pia imefanyika hivi karibuni vilevile kwa ufanithi mkubwa ambapo  mwanamziki mwanaharakati ROMA alitoa burudani ya kutosha  japo hatukuwa na pesa ya kutosha kufanya sherehe hii kama  1300000/= tu ilitumika kuratibu yote mliyoyaona sikuj hiyo.

Saba, timu zetu za football, netball, basketball zilifanya ziara chuo kikuu cha  Dar es salaam kwa michezo ya kirafiki kwa ujumla  tulifanya vema na kumpa furaha mkuu wa chuo ambaye ametoa ufadhili kwa wale waliofunga magoli.

Nane, tumenunua vifaa vya michezo vilivyo bora zaidi kwa ajili  ya timu zetu

Tisa,  timu yetu ya football imefanya michezo mingi ya kirafiki dhidi ya ya bugando na  toto na kushinda thidi ya Bugando kutoa droo kwa toto  inayoshiriki ligi kuu (pongezi).

Kumi, kwa mara ya kwanza tumeweza  kushawishi viwanja vyetu; kwanza kuwekwa eneo  na pia kufanyiwa marekebisho makubwa. Kwa sasa uwanja ni basketball umefanywa matengenezo makubwa uwanja wa netball pia umefanyiwa marekebisho makumbwa uwanja wa football pia umefanyiwa marekebisho makubwa na pia ujwanja wa netball umejengwa upya karibu na raila odinga

Kuhusu usafiri na mawasiliano serikali yetu imefanya yafuatayo:-

Mosi mpango wetu wa kununua gari (basi) kubwa umezaa  matunda  ambapo VC amepata msaada wa basi katika moja ya nchi aliyotembelea huko ulaya taratibu za kulileta hapa zinaendelea

Tumeweza kutengeneza na kuweka masanduku ya maoni, sehemu mbalimbali kantini, SAUTSO na karibu na  M13 ili kupokea  maoni  na kama sehemu ya kuwajibika  kwa kuwa wawazi, maoni mengi na  mbalimbali yametolewa na  tumeyafanyia kazi. Tunamalizia taratibu za kutengeneza natice  bodi bora na ya kisasa.

Changamoto bado ni nyingi sana;

Bado baadhi ya ndugu zetu hawapati mikopo kwa wakati, ieleweke si tatizo la serikali yangu bali uzembe wa board na wanafunzi we nyewe, ikiwemo na uzembe wa baadhi ya watumishi wa chuo

Pia kuna uchache wa madarasa jambo linalopelekea kuwa na vipindi hadi jumamosi, baadhi ya programme hazina walimu wa kutosha

Baadhi ya madarasa yapo karibu na barabara hivyo kelele za magari na wapiti njia ni tatizo

Gharama za makazi ni changamoto nyingine japo ni ya muda tu kwani naamini kwa mwaka ujao wa masomo hali itakuwa tofauti

Utaratibu wa kutoa provisional result bado hauridhishi katika ufanisi  na kasi ya kutoa.

Bado  baadhi ya watumishi wa chuo hawathamini nafasi ya mwanafunzi na serikali ya wanafunzi kwa ujumla, hoja ,kero,ajenda na maombi mbalimbali ya wanafunzi kupuuzwa bila kujali kuwa uwepo wao si lolote kama si sisi wanafunzi

 Kuhusu bylaw tumefanya kila tuliloweza lakini hadi sasa hakuna, wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawajui wanaishi katika wigo upi wa kisheria, nini haki na wajibu wao kama wanafunzi, kwa ujumla wanafunzi hawajui yako wapi mabadiliko ya bylaw yanayosemwa, corporate yupo hapa, nimefika ni zaidi ya mara nne kwake juu ya hili, Kuhusu prospectors pia corporate atakili.

Kuhusu penalty ya sh. laki moja, ndugu zangu tambueni hatukuiunga hatujaiunga na hatutaiunga kwa sababu zifuatazo; nikubwa mno,wanafunzi hawakupewa fursa na mda wa kuijua na hatimaye kujiandaa kuikabili (principle of natural justice)

Shukrani

Nawashukuru wanafuzi wenzangu wote kwa ushirikiano wenu kwangu, ushauri na pongezi zao mara zote zimeniimarisha

Nawashukuru wawakilishi wa madarasa(CRs)

Nawashukuru waheshimiwa wabunge

Nawashukuru sana makatibu wakuu,  naibu waziri, mawaziri, waziri mkuu, katibu mkuu na makamu wa raisi

Namushukuru mama Dean

Muhasibu wa chuo

DVCAA

Corporate

DVCAF

Makamu mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo.

“Tumeona tunaona na tutaona”

Asante

Cosmas kula mataba

Rais SAUTSO (2011-2012)

Mwenyekiti SUSAUT(2011-2012)

Mwenyekiti kamati sheria TAHLISO (2011)

Spika EACSU(2011-2012)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s