ELIMU YA JUU NA CHANGAMOTO YA ONGEZEKO LA GHARAMA NCHINI.

Prosper Mosha mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Shahada ya Kwanza
ya Kazi Jamii/Ustawi wa Jamii, katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii
(ISW).

UKUAJI wa kiwango cha elimu hapa nchini kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo kikuu umekuwa sio wa kiwango cha kuridhisha, na hii ni kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hii muhimu katika ukombozi wa fikra.

Jitihada kadhaa zimekuwa zikifanywa na serikali kupitia Wizara ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza, kuboresha miundombinu, kuongeza walimu na kubadilisha mitaala pale inapobidi ili kuendana na mahitaji.

Kwa kufanya hivyo haina maana mabadiliko hayo yameweza kuonekana kwa haraka bali ni mabadiliko yenye kuchukua muda ili kuona matunda yake. Hii ikiwa ni kutokana na muundo wa elimu tuliyonayo yaani kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu.

Baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hii muhimu katika ukuaji wa uchumi na maendelo ya nchi kwa ujumla ni pamoja na ukosefu wa wataalamu yaani walimu wenye sifa, mitaala iliyopitwa na wakati, na gharama kubwa za upatikanaji elimu kuanzia ngazi ya shule za awali hadi vyuo vikuu.

Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayokwamisha na kudhoofisha sekta ya elimu hapa nchini kwa baadhi ya shule za serikali na zile za binafsi hivyo kuifanya sekta hii mama kuendelea kupoteza uwezo na sifa.

Hili linadhihirika pale watanzania wanapoamua kusomesha watoto wao tangu shule za awali, msingi, sekondari hadi chuo kikuu nchi za nje tena jirani zetu kama Kenya na Uganda; Hii ni fedheha kubwa kwa taifa letu.

Baadhi ya wahitimu wa ISW wakiwa kwenye hafla ya mahafali.

Lakini pia wazazi wengi wamekuwa wakifanya hivi kutokana na ukubwa wa gharama za elimu wanazopaswa kulipia hapa nchini na kiwango cha elimu anachodhania nakuona kuwa haviendani hivyo anadhiriki kutumia gharama kubwa akiithaminisha na ubora wa elimu anayoitarajia nchi za nje ambayo inaweza kuwa inaendana kweli au lah.

Prosper Mosha ni mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Shahada ya Kwanza ya Kazi Jamii/Ustawi wa Jamii, katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Dar es Salaam anazungumzia ukubwa wa gharama has za elimu juu ilivyo baguzi na yenye kujenga matabaka kati ya wenye ahueni ya maisha na wale walalahoi au wakulima.

Anaanza kwa kutoa mifano kama Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambavyo kwa katika ya kipindi cha mwaka wa masomo 2009/2010 na 2010/2011ni kati ya vyuo vilivyoamua kuongeza gharama za masomo licha ya wanafunzi hao kuwa tayari walishaanza masomo hivyo mpango huo kuwaathiri.

Mosha anasema ongezeko hilo la gharama za ada wakati mwingine limekuwa halizingatii makubaliano katika ya wanafunzi na uongozi wa chuo husika hivyo kuwashtukiza wanafunzi bila kujali hali za familia walizotoka ikizingatiwa kuwa wengi wao ni watoto wa wakulima, wamachinga, wafugaji katika hali za chini za maisha.

“Vitendo hivyo bila kujali vimekuwa vikiwaathiri wanafunzi wengi hata baadhi yao kukatisha masomo hasa kwa kukusa namna ya kuendelea kulipa kiwango cha ada kilichozidi… imekuwa ikiwafanya kujiingiza kwenye migomo, vurugu na uchochezi hali inayohatarisha amani na uharibifu mkubwa! Tumeshuhudia hayo,” anasema.

Anaongeza kawa Bodi ya Mikopo ya ELimu ya Juu (HESLB) imekuwa haijihusishi kwa namna yoyote na ongezeko hilo la ghafla la ada kutokana na kutokuwa na mawasiliano na dmakubaliano mazuri baina ya uongozi wa vyuo hivyo na uongozi wa HESLB hivyo mzigo huo kuwaelemea wanafunzi na wazazi wao.

Mosha anasema amekuwa akifatilia kwa makini (siyo rasmi) baadhi ya migogoro inayojitokeza katika baadhi ya vyuo vya elimu ya juu na kubaini mingi ya migogoro hiyo chanzo chake ni ugumu na ukata wa maisha unaowakabili wanafunzi wawapo vyuoni kwa kushindwa kumudu gharama za maisha ambayo hutokana na gharama kubwa wanazolipa na usumbufu kama huo wa ongezeko la ada wakatiw akiwa tayari wameshajisajili wakiendelea na masomo.

Ni wengi katik yetu tumewahi kusikia wanafunzi waelimu ya juu kwa wasichana wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya ngono, kujiuza na makosa mengine huku wakiume wakati mwingine kuhusishwa na uvutaji na uuzaji madawa ya kulevya, hii yote ni jitihada za kutaka kunusuru maisha yao hivyo ongezeko la gharama za shule kama ada ni wazi kuwa hauendani na gharama zao za maisha.

“Unakuta mwanafunzi kwao alikozaliwa familia yake inakula milo miwili tena ya wasiwasi kwa siku wazazi wake wamejinyima amefanikiwa kupata hicho alichoweza, leo unapandisha hizo gharama na hana uhakika wa kupata kutoka nyumbani kwao huyu mtu ataacha kuiba, kuwa changudoa ilimradi tu apate chochote kimsaidie kumalizia ada yake? Alihoji Mosha.

Anaongeza kuwa gharama hizi zimekuwa haziwiani na huduma za elimu inayotolewa kwani kumekuwapo na gharama zingine za ziada ambazo wahadhiri wamekuwa wakiwatoza wanafunzi wakidai kuwa wanawafundisha muda wa ziada (overtime), na kununua vijitabu vidogovidogo, hii yote haimuangalii huyu mwanafunzi hali yake ya maisha ikoje!

Hili linakwenda sambamba na baadhi ya vyuo hivyo hapa nchini kama Chuo Kikuu cha Kampala kilivyokuwa kikitoza ada kwa kutumia malipo ya fedha za kingeni U$D kitendo kinachotufanya tuzidi kuidharau elimu yetu, yani hata mgeni yupo kwetu anatupangia utaratibu wake tunaufuata na anaamua kutetesa vilevile…maana tumeshindwa kusimamia mabo ya msingi katika kukuza elimu yetu hivyo tusilishangae hilo!

Bw. Mosha anaelekeza kilio chake na kuzishauri mamlaka husika kama Serikali, Uongozi wa Taasisi na Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu hapa nchini kuona haja ya kutumia mbinu shirikishi kwa wanafunzi hasa katika suala hili zito kwani litawafanya hata kubadili namna yao ya upokeaji hivyo kutojihusisha na migomo ya kuipinga badala yake iwe ni mauzngumzo ya makubaliano.

Serikali ndie msimamizi mkuu wa mambo yote hivyo huduma hii inayotolewa na watu binafsi na kujiendesha kimabavu Serikali inapaswa kulitupia macho na kukemea kwa kuweka utaratibu unaeleweka wa viwango vya ada, mbona kwenye huduma zingine kama viwango vya kununua mafuta ya taa, Petrol, na Disel imewezekana!

Anatolea mfano wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii aliposoma na kuhitimu shahada yake kwa kusema kuwa ni chuo cha Serikali na kwa muda mrefu sasa hakijandisha ada kwa kozi na ngazi zote, Je chenyewe kinatofauti gani na vyuo vingine? Au kuwepo ongezeko la ada mara kwa mara ni ishara kuwa ndipo penye elimu bora? Amewataka pia wadau wa elimu kuingilia kati suala hili na kulipigia kelele kwani vinginevyo elimu ya kitanzania itatushinda kuinunua kwa gharama hiyo inayopaa.

Short URL: http://www.thehabari.com/?p=11330

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s