WANAFUNZI ST. JOHN DODOMA WAANZA KUSAINI FEDHA ZAO ZA MIKOPO.

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John mkoani dodoma, juzi jioni walianza kazi ya kusaini vocha za malipo ili kupatiwa fedha za kujikimu zitakapofika chuoni hapo kutoka  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Awali wanafunzi hao waliitisha mgomo na kugoma kusaini majina yao na kusubiri fedha kutoka Bodi ya Mikopo kufika chuoni kwa madai kuwa chuo kilikuwa kimepokea fedha.

Hata hivyo, chuo kilikanusha kupokea fedha kutoka Bodi ya Mikopo ila kilichokuwa kimefika chuoni hapo ni majina tu ya wanafunzi waliostahili kulipwa.

Akizungumza na gazeti hili jana chuoni hapo, Katibu wa Serikali ya Wanachuo, Isidory Msuva alisema kazi hiyo ambayo ilianza juzi saa moja usiku, inaendelea vizuri.

Alisema wanafunzi wanaendelea kusaini ili fedha zitakapokuja waingiziwe kwenye akaunti zao moja kwa moja.

“Zoezi linaendelea vizuri juzi saa moja usiku wanafunzi walianza kusaini chini ya ulinzi wa polisi kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), baada ya kukubaliana na Viongozi wa Chuo na Serikali ya Wanachuo, lakini leo hakuna ulinzi wowote wa polisi na zoezi linaendelea vizuri” alisema Msuva.

Alisema jumla ya wanachuo 2,400 wako kwenye kazi ya kusaini vocha za malipo na Bodi ya Mikopo mkoani hapa imeahidi kuingiza fedha hizo mapema zaidi ili wanafunzi hao waanze
kulipwa.

Vurugu zilitokea chuoni hapo juzi baada ya kubandikwa notisi iliyowataka wanafunzi kusaini na kisha fedha zingetolewa baada ya fedha kuwasili chuoni hapo.

Kwa mujibu wa notisi hiyo iliyotolewa Desemba 19, mwaka huu, chuo hakijapokea fedha za robo ya pili ya fedha za kujikimu zilizotolewa na Bodi na imeahidi itaziweka kwenye akaunti ya chuo ndani ya wiki hii.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s