VODACOM YACHANGISHA SH. MIL 6,284,000 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR.

Baadhi ya waokoaji wakiwaokoa waathirika wa mafuriko siku ya maafa.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania inawashukuru wote ambao tayari wameshaonyesha upendo wao kupitia kampeni ya “Red Alert” na kufanikisha kukusanya shilingi 6,284,000/= kati ya December 22, 2011 hadi December 27, 2011.

Tunapenda kutoa wito wa kuendelea kuchangia Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko kwani bado wanahitaji misaada yetu, kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS yenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.


Jinsi ya kuchangia kwa M-Pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za M-Pesa. Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
 Hatua ya 7: Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s