MWANAFUNZI ALIYETIMULIWA ST. JOHN ADAKWA AKITAKA KUJISAJILI.

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St. John mkoani dodoma, jana walianza kujisajili huku mwanafunzi mmoja aliyesimamishwa masomo akikamatwa baada ya kujipenyeza ili asajiliwe. 

Hata hivyo, shughuli hiyo ilichelewa kuanza ambapo msemaji wa chuo hicho, Karim Meshack alisema kuwa, walikuwa wakisubiri ulinzi kutoka Polisi.

Wakati wanafunzi hao wakisajili mwanafunzi mmoja Ayub Benjamini wa Shahada ya Elimu, aliyekuwa miongoni mwa wanafunzi 15 waliosimamishwa alijipenyeza ili asajiliwe.

Hata hivyo, Benjamini aligundulika na polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia waliokuwepo uwanjani hapo walimkamata na kumuweka chini ya ulinzi.

“Kazi inakwenda vizuri ingawa ilichelewa kuanza kwa vile tulikuwa hatujapata ulinzi, lakini kila kitu kinakwenda vizuri na tunategemea kesho tutamaliza na kesho kutwa masomo yataanza,” alisema Meshack.

Alisema kuwa kila mwanafunzi anatakiwa kulipa ada ya Sh 5,000 katika usajili huo na hakuna tatizo lolote lililojitokeza zaidi ya kukamatwa kwa mwanafunzi ambaye alikuwa hana sifa za
kusajiliwa.

“Ni kweli mwanafunzi huyo amekamatwa na yuko chini ya ulinzi kwa hatua zaidi,” alisema.

Wanafunzi wanaokaribia 4,000 walikuwa wakisubiri kusajiliwa baada ya chuo hicho kufungwa Desemba 23, mwaka jana kwa sababu ya vurugu za madai ya fedha za kujikimu kutoka Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu (HESLB).

Tayari wanafunzi hao wameshalipwa madai hayo baada ya kuingiziwa fedha kupitia akaunti zao.

Habarileo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s