DIAMOND NA WENZAKE WAFUNGWA JELA MIEZI SITA IRINGA.

Diamond akionyesha mbwembwe baada ya kuwasili mahakamni hapo akiwa na mcheza shoo wake.

Mdhamini wa msanii DIamond Edo Bashir Kushoto akizungumza na mmiliki wa mtandao huu Francis Godwin ambaye ndie mlalamikaji katika kesi hiyo.

Diamond akiingia mahakamani.

MSANII nyota wa muziki wa Kizazi kipya nchini Naseeb Abdul a.k.a Diamond na wenzake jana mjini Iringa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya sh. 50.000 kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari mkoani Iringa Francis Godwin.

Godwin ambaye pia ni mmiliki wa Blog ya Francis Godwin, hajaridhika na hukumu hiyo na tayari amekata rufaa na ataenda katika mahakama ya juu. Hukumu hiyo imekuja baada ya msanii Diamond na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya mahakama kuwa yeye na wenzake walitenda kosa hilo na kuharibu Camera mbili, Lap top aina ya Accer pamoja na kumshambulia Godwin Desemba 31 mwaka jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Hakimu Masua alisema kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu kwenda jela miezi 6 au kulipa fidia ya sh. 50,000 kila mmoja na huku wakilazimika kumlipa Godwin pia sh. 30,000 kila mmoja na kufanya kufikia kiasi cha sh. 90,000.

Wakitoa utetezi wao watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia adhabu kwa kuwa hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja mkoani hapa kwa ajili ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo wamelifanya kwa ghadhabu.

Hata hivyo watuhumiwa wamelipa faini japo mmiliki wa mtandao huo, Godwin hajapokea fedha hiyo na amekusudia kukata rufaa na kwenda katika mahakama ya juu zaidi, kwa kile kutoridhika na hukumu iliyotolewa dhidi ya wahusika.

Diamond ambaye ni msanii chipukizi ambaye amekuja juu kwa kasi kutokana na kukubalika kwake na hata kufanikiwa kuwa msanii wa kwanza kupata tunzo tatu katika sherehe za kuwatunuku wasanii za Tanzania Music Awards 2010, zilizofanyika mwaka 2011, kwa sasa ameandamwa na matukio kadhaa ya mahusiano ambayo yamemfanya jina lake kuendelea kutajwa mara zote katika vyombo vya habari.
Chanzo: Francis Godwin Blog

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s