KUTOKA UDOM: WANAFUNZI WASAIDIA WAJAWAZITO.

WANAFUNZI wa Kitivo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana walikabidhi misaada kwa wajawazito wanaosubiri kujifungua waliopo katika Kituo cha Chikande, jirani na Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma.

Misaada iliyokabidhiwa, yote ikiwa na thamani ya Sh 300,000 ni pamoja na mchele, sembe, mafuta ya kula, peremende, majani ya chai, sabuni, dawa za meno na mafuta ya kupaka.

Akikabidhi misaada hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Kombo Mwishashi alisema badala ya wanafunzi kujihusisha na migomo ambayo wakati mwingine haina ulazima, pia wana nafasi kusaidia jamii kwa njia mbalimbali.

“Tumeona ni bora kuwasaidia watu walio katika mazingira magumu kama hawa akina mama wajawazito wanaokosa huduma muhimu huku wakisubiria muda wa kujifungua,” alisema Mwishashi.

Aliongeza kuwa, wanafunzi hao wameguswa na masuala ya akinamama wajawazito ambao wanalala chini kutokana na vitanda vichache na kusababisha msongamano huku wengine wakilala wanne katika kitanda kimoja.

“Hivyo tumeona umuhimu wao ndio maana tumekuja kutoa misaada hii japokuwa ni kidogo na hatuoni kama kuna maana ya kuitwa wasomi ambao hawajihusishi na masuala ya jamii inayotuzunguka badala yake wanashabikia migomo na maandamano, ”alisema Mwishashi.

Aidha alitoa rai kwa wasomi kuacha migomo ya mara kwa mara inayoendelea na badala yake wajihusishe kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamiii. “Imefika wakati wa kutumia elimu tuliyonayo kwa kuleta manufaa katika jamii na kuachana na migomo ambayo inatupotezea muda mwingi,” alisema Mwishashi.

Alitoa wito kwa wasomi kujifunza mahitaji na matatizo yanayokabili jamii na kutumia fursa za kitaaluma kufanya utafiti na kuwapatia ufumbuzi kwa matatizo wanayokumbana nayo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s