PINDA KUTUNUKU VYETI CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ACT).

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya tatu ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa chuo hicho, Dk. Richard Masika, Waziri Mkuu anatarajiwa kutoa vyeti kwa wahitimu wapatao 231.

Alifafanua kuwa, kuwa miongoni mwa wahitimu hao, 40 ni wa ufundi sanifu wa ujenzi, 46 wamehitimu ufundi sanifu umeme na 45 ni wahitimu wa fani ya ufundi sanifu katika fani ya elektroniki na mawasiliano ya anga.

Aidha amefafanua kwamba wahitimu 36 ni wa fani ya ufundi sanifu usafirishaji, 31 ufundi sanifu mitambo na wahitimu wapatao 33 ni wa fani ya ufundi sanifu magari.

Mkuu huyo wa chuo ameeleza kuwa Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa wataalamu wa kada ya mafundi sanifu wenye elimu ya ufundi sanifu wenye uwezo kiutendaji hususani katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo ya umwagiliaji

Amesisitiza kuwa wahitimu hao watasaidia kupunguza matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayolikabili taifa hivi sasa , matatizo ambayo yanachania kuwepo na uzalishaji duni katika sekta ya viwanda

Dk. Masika amefafanua kuwa wahitimu hao watasaidia kupunguza matatizo katika programu ya uhandisi ujenzi umwagiliaji ambapo wataweza kusanifu na kusimamia ujenzi wa skimu za umwagiliaji nchini katika sekta ya kilimo.

Hata hivyo, Dk. Masika alisema mbali na kuwa mahafali hiyo ni ya tatu, lakini ni ya 30 tangu chuo hicho kianzishwe mwaka 1978 kabla ya Serikali kukifanyia mabadiliko rasmi mwaka 2007.

Aidha, Dk. Masika alieleza kuwa tangu mwaka 2007 na 2011 chuo hicho kimefanikiwa kuongeza programu kutoka sita hadi 11 ikiwa ni ongezeko la asilimia 83.

Mahafali hayo pia yanatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Wajumbe wa Bodi ya Utawala ya chuo hicho, mabalozi pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na madhehebu ya dini.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s