KUTOKA MSJ: WANAFUNZI WAPINGA UVAAJI VIMINI CHUONI CHUO CHA UANDISHI WA HABARI MOROGORO

KAMPENI ya kupinga mavazi yasiyo na heshima imeendelea kushika kasi na kusambaa katika baadhi ya vyuo ambapo kwa mara nyingine tena imejitokeza wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ).

Waanzilishi wa kampeni hiyo ni Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na siku chache zilizofuatia Chuo Kikuu cha Tumaini, Kampasi ya Dar es Salaam ilipanga kutoa rasmi mwongozi kuhusiana na jambo hilo.

Katika mahafali hayo ya 15 ya MSJ, wanafunzi wa chuo hicho kikongwe cha binafsi, nao wamelaani vikali tabia ya uvaaji wa mavazi hayo kupitia ushairi wao waliousoma wakati wa hafla hiyo.

Wanafunzi wa chuo hicho walipobainisha hayo wakighani shairi kwenye mahafali hayo yaliyofanyika Machi 31, mwaka huu katika Ukumbi wa JKT Nane Nane mjini hapa.

Wakisoma shairi hilo mbele ya mgeni rasmi Katibu wa Baraza la Habari Tanzania ( MCT) Kajubi Mkajanga na viongozi wengine kwenye mahafali hayo, waghani wa shairi hilo pamoja na kuzungumzia mambo mengine, ubeti wa nane ulilaani nguo fupi zinazovaliwa mwilini na baadhi ya wasichana wakiwemo wanafunzi wenzao.

Pamoja na kulaani uvaaji wa nguo fupi na vimini, wanafunzi wa chuo hicho walitumia fursa hiyo kuwaasa wahitimu wa mahafali hayo na watu wengine wachukue tahadhari juu ya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna kinga wala dawa na haujali rika.

Jumla ya wahitimu 139 wa fani ya uandishi wa habari ngazi ya cheti na diploma, pamoja na walimu wa shule za awali walitunukiwa na mgeni rasmi.

Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Said Dogoli alisema tangu kianzishwe miaka 17 iliyopita wahitimu 716 wa masomo ya Uandishi wa Habari wamesoma chuoni hapo na wengi wamepata ajira katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya Serikali na sekta binafsi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s