NI WATANZANIA WANGAPI WANAJUA THAMANI YA KURA?

Nchini Tanzania kumekuwa tatizo kubwa la watu wanaojiandikisha kupiga kura kutokujitokeza kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi, kuna sababu nyingi zinazoweza kuwa zinachangia hali hiyo.Mwandishi Wetu anachambua utafiti uliofanywa na Kituo cha Taarifa kwa Wananchi.

Kituo hicho kinasema ili watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura lazima kuwe na programu endelevu ya utoaji wa elimu ya uchaguzi kwa miaka yote na kuwahamasisha wafadhili kutoa ufadhili kwa wakati wote wasisubiri kipindi cha uchaguzi mkuu tu.

Kinasema kwa kufanya hivyo wananchi watapata fursa ya kuelimika sanjari na kupata ufahamu mbalimbali wa masuala ya uchaguzi na siasa kwa ujumla.

Hivi sasa wananchi wengi hawajitokezi kupiga kura, tatizo kubwa likiwa ni kukosa elimu hasa ya thamani ya kura yake.

Kituo kinasema vijana waanze kutumia kura yao vyema kwa kutambua umuhimu wao wakati wa uchaguzi.

Kinasema vijana ndio wanategemewa kuleta mabadiliko lakini kura zao zimekuwa zikipotea kwa kutojiandikisha ama kupiga kura badala yake wamekuwa wkaishinda wakilalamika vijiweni.

Kituo hicho kinasema vyama vya siasa lazima viangalie uwezekano wa kuunganisha nguvu kwa kuungana kwani hali hiyo italeta ushindani na hamasa ya kisiasa kwa wananchi kwa kuunganisha vyama vyenye malengo yanayofanana.

Kinasema vyama viteuwe wanawake kugombea nafasi zaidi kwani utafiti unaonyesha kuwa wapiga kura wengi ni wanawake na vijana hivyo ni vyema wakachukua fursa hiyo.

Kinasema ni vyema vyama vikawateua kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya urais, ubunge , udiwani na hata serikali za mitaa ili kuleta ushindani wa tija kwa wananchi katika chaguzi za hapa nchini.

Hata hivyo utafiti huo umepata taarifa muhimu juu ya mwitikio mdogo wa wapiga kura katika Tanzania Bara na sababu zake na kusema iko haja ya kufanya utafiti zaidi juu ya sababu zinzofanya Zanzibar kuwa na mwitikio mkubwa zaidi kuliko Bara wakati baadhi ya sheria na sera za uchaguzi zinafanana sana.

Utafiti umeonyesha kuwa umasikini na ukosefu wa ajira kwa vijana ni moja ya sababu zilizowafanya watanzania wengi kushindwa kujitokeza kupiga kura katika chaguzi mbalimbali.

Kadhalika, utafiti huo umebaini sababu zingine kuwa ni pamoja vitisho kutoka vyombo vya dola, imani za kishirikina na wananchi kutoiamini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Deus Kibamba, alipotoa taarifa juu ya matatizo na kero ambazo zinawakabili watanzania kushindwa kujitokeza kupiga kura kuwa vitisho pamoja na matumizi mabaya ya dola katika uchaguzi yamekuwa siyo rafiki kwa mpigakura.

Akitolea mfano wa namna askari polisi wanavyovaa wakati wa upigaji kura kana kwamba wanakwenda vitani na kusema hali hiyo imekuwa ikiwatia hofu wananchi na hivyo kushindwa kujitokeza kupiga kura.

Jeshi la Polisi linatakiwa kubuni mbinu mbadala na kuimarisha ulinzi katika vituo vya kupigia kura kwani huvaa mavazi ambayo huashiria kuvunjika kwa amani eneo husika ikiwemo kuwa na silaha za moto ni miongoni mwa kero mojawapo ya kutohamasisha wapiga kura na badala yake wananapaswa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi hasa wakati wa uchaguzi.

Chaguzi nyingi nchini zimejawa na imani za kishirikina, na kupelekea sehumu kubwa ya vijana ambayo kimsingi ndiyo wapiga kura wakihofia suala hilo, baadhi ya maeneo kama Shinyanga wamekuwa wakitishwa kwamba endapo hawatachagua mgombea wa chama fulani basi watapatwa na ugonjwa wa Ngilimaji (busha).

Hata hivyo, anasema tume ya uchaguzi NEC imekuwa kikwazo na kulalamikiwa na wananchi kwa kutoona majina yao kwa usahihi na kupata usumbufu ambao unawapelekea kutokuona umuhimi wa upigajikura.

“Ufutaji wa majina katika daftari la wapiga kura bila utaratibu kwa mwaka 2009-2010 tumeilibaini majina 256,000 yaliandikishwa mara mbili na badala ya kupitia jina kwa jina kugundua sababu, Tume iliamua kufuta majina yote na kuleta usumbufu kwa wapiga kura” alisema Kibamba

Kwa upande wake Kiongozi wa Utafiti Jacqueline Materu, alisema mapendekezo yao ni mabadiliko yafanyike katika NEC ili wananchi waweze kuwa na imani upya na tume, kuundwa kwa sheria ambayo itaimarisha uhuru kwa watu wakienda kupiga kura wawe huru.

“Tume ipate wawakailishi na watendaji kutoka kwenye kata isiishie kwenye majimbo tu hii itasaidia kupata taarifa kwa urahisi na sahihi,” alisema Materu

Tafiti hiyo imebaini kuwa tatizo la watanzania wengi kukosa fursa ya kupiga kura linakuwa kwa kasi kulinganiasha miaka ya 1960 na 1990 ambapo mwaka 2010 tatizo hilo lilikuwa kubwa kiasi kwamba hata nusu ya wapiga kura haikufika.

Takwimu zinaonyesha kuwa wapigakura 20,000,000 waliyojiandikisha katika daftari ya wapiga kura (PNVR) ni 8,626,283 sawa na asilimia 42 tu ndiyo waliweza kujitokeza kupiga kura kitaifa.

Kwa upande wa majimbo, Segerea (DSM) kati ya 341,718 walioandikishwa ni watu 104,376 sawa na asilimia 30.5 ndiyo waliweza kupiga kura, Njombe Kusini (Iringa) kati ya 75,383 walioandikishwa ni watu 30,000 ndiyo waliweza kupiga kura, Bukoba mjini (Kagera) 77,554 ni watu 33,000 ndiyo wameweza kupiga kura, Mtwara mjini kati ya 69,373 ni watu 30,000 pekee ndiyo walipiga kura na Babati mjini (Manyara), kati ya 35,362 ni watu 20,916 walioweza kupiga kura.

Tafiti hiyo imebaini kuwa miaka ya nyuma watu walikuwa wakijitokeza kwa wingi hadi kufikia asilimia 76.6 ya watu waliopiga kura mwaka 1995 kati ya watu 8,929,000, mwaka 2000 kati ya watu 10,088,000 waliyojiandikisha zaidi ya asilimia 84.4 waliweza kupiga kura, mwaka 2005 waliojiandikisha ni watu 11,875,000 na zaidi ya 72.4 waliweza kupiga kura na mwaka 2010 ilikuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kupata asilimia 42.8 kati ya jumla ya wapiga kura 19,694,055 waliyojiandikisha Tanzania Bara.

Aidha, hali hiyo ya watanzania kutojitokeza kupiga kura iliendelea zaidi kwa wingi katika uchaguzi mdogo Igunga kwani kati ya watu171,019 waliyojiandikisha kupiga kura ni watu 56,072 walioweza kupiga kura sawa na asilimia 33.

Utafiti huo baada ya kubaini kero na vikwazo zinavyowakabili watanzania kuachakujitokeza kwa wingi miongoni mwa matokeo na maependekezo ni marekebisho ya mfumo wa upashanaji na usambazaji taarifa kati kati ya waratibu wa uchaguzi ikiwemo Tume ya Uchaguzi Taifa NEC na wananchi ni hafifu.

Changamoto za Tume ni nyingi ikiwemo tatizo la kimuundo, watendaji, vifaa na uhuru wautendaji kazi kiasi kwamba watu wengi wamepoteza imani na NEC, rushwa nje nje wakati wa uchaguzi na kupelekea wapiga kura wasiofikiwa na fedha kutoona umuhimu wa kupiga kura, wawakilishi wa tume ipo haja ya kuwa na watu hadi kwenye kata na kuondoa malalamiko kwa wapiga kura yasiyo ya lazima ikiwemo vitisho, mfano mtu asipopigia kura mgombea wetu wakati amekula pesa zetu atajikuta kwenye shimo la choo (Mlandizi).

Tafiti hiyo imetoa mependekezo mengi kwa NEC kuanzishwe na Kituo cha Taarifa za Uchaguzi ilikutoa taarifa zote muhimu zipatikane hapo na kwa uwazi sanjari na vyombo vya habari kutoa elimu juu ya uchaguzi mfululizo pasipo kusubiri wakati wa uchaguzi.

Pia kinasema NEC iundiwe sheria ambayo itamsaidi mpiga kura kumpa imani zaidi, Mfano Tume ya Uchanguzi Zanzibar kwa NEC kuhusu wajumbe kadhaa kutoka makundi ya kijamii pia NEC ipate watendaji wake kutoka ngazi ya taifa hadi kwenye kata.

Kinasema Msajiri wa vyama vya siasa aweke utaratibu wa utoaji ruzuku kwa vyama vyote ili uchaguzi uwe wa ushindani zaidi na kuondoa zaidi ushindani wa vyama vichache. Mfano kuna chama kinapata ruzuku ya bilioni 1 kwa mwezi na vingine milioni 100 wakati vyama zaidi ya 10 havipati chochote.

Kituo hicho kimependekeza kuwe na mgombea binafsi ili kuongeza hamasa ya watu wengi kushiriki chaguzi hasa pale endapo vyama vitateuwa wagombea wasiokubalika na wakati mwingine kuna kuwa na watu wanaotaka kugombea lakini hawataki kupitia vyama vya siasa.

“ Bunge la Tanzania halina sababu ya kusuasua kuhusu mgombea binafsi kwani baada ya hukumu ya Mahakama ya Rufaa ambayo sasa imeacha suala hilo mikononi mwa Bunge pekee,” ilisema sehemu ya mapendekezo katika utafiti huo.

Vyama vya siasa vimeshauriwa kuhamasisha wapika kura juu ya ushiriki wa uchaguzi ikiwemo kuwahamasisha wakajiandikishe, vyama viepuke kuwahamasisha wananchi kutoshiriki katika mikutano ya hadhara ya vyama vingine ili kuepuka kuondoa hamasa na ushindani wa uchaguzi.

Utafiti huo wa mwaka mmoja, kuanzia Januari,2011 hadi Februari, 2012 uliofanywa katika Wilaya 13 za mikoa 13 nchini Tanzania Bara na Visiwani ikiwemo Mwanza, Shinyanga,Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Coast, Wete,Pemba, Iringa Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Dodoma.

Watu 1,600 walihojiwa katika Wilaya 13 wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 75 kati ya hao ushiriki wa wanawake ni asilimia 42 kulinganishwa na wanaume 58.
SOURCE: NIPASHE

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s