KUTOKA CHUO KIKUU CHA ARDHI: KAMPENI ZA UCHAGUZI KUWANIA UONGOZI KATIKA SERIKALI YA WANAFUNZI ZAENDELEA KWA MBWEMBWE.

Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Ardhi (ARUSO) imemaliza muda wake na hivyo iko katika mchakato wa kutafuta Rais mpya wa serikali hiyo pamoja na wabunge watakaongoza serikali hiyo kwa kipindi cha 2012/13 Chuoni hapo.

Aidha kampeni za mgombea Urais ndugu Enock Tarimo zimeonekana  kuwawavutia wanafunzi wengi kwani amekuwa akitembelea wapiga kura wake huku akiwa ameandamana na walinzi wake ambao wamekuwa wakimlinda kila anapokwenda. Aidha mgombea huyo Bw. Enock Tarimo ndie ambae anaonekana ni mwenye asilimia kubwa ya kuweza kushinda katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu wa nne chuoni hapo. Wagembea wengine ni; KIDAI,Joseph pamoja na CHACHA,Matiku.

Raisi mstaafu wa serikali ya wanafunzi ARUSO Mh.Ismail Mvungi akipeana mkono na mgombea huyo (Mwenye suti) Bw. Enock Tarimo.

Mh.Enock Tarimo (Mwenye suti)akijiandaa kuanza mizunguko yake ya kampeni zake na mabodyguard nyuma wakitoa ulinzi mkali.

Hiyo ni moja ya kazi za hawa walinzi wa Bw. Tarimo pale anapokuwa amechoka basi wao hugeuka kuwa usafiri ili mradi kuleta hamasa kwa wafuasi wa mgombea wao. Hapa ni katika maeneo ya Survey jiijini Dar es salaam karibu kabisa na Chuo cha Ardhi ambapo wanafunzi wengi huishi maeneo hayo. Bw. Tarimo hufanya kutembelea katika makazi ya wapiga kura wake ili kuwaelezea kwanini yeye anafaa kuwaongoza.

MICHEZO NI MUHIMU KWA AFYA ZETU KAMA WASOMI: Hapa Ndugu Tarimo akiwasalimia wanamichezo katika kampeni zake katika fainali ya michuano ya chuoni hapo..

NAOMBA KURA ZENU NDUGU ZANGU: Bw. Tarimo alisikika akisema hayo kwa wapiga kura wake.

Wafuasi wa Bw. Enock Tarimo wakimshangilia mgombea wao katina kampeni zake.

HUU SI MGOMO WA MIKOPO BALI NI KAMPENI ZA URAIS KATIKA CHUO CHA ARDHI...Ilikuwa ni katika mitaa ya Chuo Kikuu cha Ardhi pale wafuasi wa Ngd. Enock Tarimo walipokuwa wakimpa nguvu mgombea wao.

Advertisements

2 responses to “KUTOKA CHUO KIKUU CHA ARDHI: KAMPENI ZA UCHAGUZI KUWANIA UONGOZI KATIKA SERIKALI YA WANAFUNZI ZAENDELEA KWA MBWEMBWE.

  1. hujui chochote wewe! huyo mgombea unayempigia kampeni anakubalika na skuli yake ya sres tu na uhakika wa kushinda kwake ni mdogo sana. kama umetumwa uwe na vivid example! hyo ni aibu. HATUMTAK1 kwani amewekwa na administration.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s