VIDEO YA MBUNGE WA MTERA (CCM) LIVINGSTONE LUSINDE AKIWATUKANA CHADEMA

Mbunge wa Jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akimwaga sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Viwanja vya Ngarasero katika Kata ya USA River Wilayani Arumeru. Mkutano huo ulifanyika tarehe 26/03/2012 saa 9 Alasiri.

IMPACT OF SOCIAL MEDIA IN OUR DAY-TO-DAY LIFES.

In the wake of accepting technological advancements, we’ve also come to embrace the term ‘social-networking.’ Starting as an easy way of communication, social networks have accelerated their pace towards transmogrifying our lives. Whether at the comfort of our homes or while commuting, they have become the intruders in our PC screens, mobile devices and our lives. They’ve brought in varied changes in the way we socialize.

Let’s discuss a few impacts that the trend of social networking has brought in:

Communication:

Social networking has changed the way we’d once communicate with friends and family. Social sites have becomes a primary means of communication with Facebook topping the list. It introduces effortless communication with someone on the opposite end of the globe. Its not just mere communication, finding a long lost friend, sending invitations, sharing pictures, letting everyone know what’s on your mind is all made quite simple.

Teenagers:

Teenagers often tend to accept and adapt to a new, trendy, tech-savvy lifestyle easily. Seemingly, social sites have a greater impact on their lives. Quality times spend by them tweeting or updating statuses won’t be a surprising fact. Nevertheless, it has been used by collegians to spread good and meaningful messages.

Recruitment:

Recruitment is another factor that has been quite responsive to the ongoing social media phase (which is here to stay). The wider reach and entering a particular class or forum to pick the right candidate is said to be one of the key reasons. Recruitment by using these social channels have been quite effective, albeit everything comes with a fair share of pros and cons.

Marketing/Advertisement:

Needless to say, social sites serve as a good way to promote products. They’ve emerged as a new marketing platform. Celebs have also been leveraging on these sites to showcase their upcoming events, albums and movies. This latest marketing/advertising platform has forked out paths to newer revenue opportunities.

Entertainment:

Social sites have becomes a part of our lives. They come as a complete package to keep one engaged with factors besides communication. Playing games and then flaunting your high scores is made possible with just a few clicks. It’s a virtual world cocooned within your device screens which opens up as a complete entertainer. People look for more ease and doing things within their comfort zone. They are wowed by the virtual world concept.

Just as a coin has two sides, social networks have their shades of white and grey. While binding the world closer and closer, they bring in bountiful changes.

KUTOKA MSJ: WANAFUNZI WAPINGA UVAAJI VIMINI CHUONI CHUO CHA UANDISHI WA HABARI MOROGORO

KAMPENI ya kupinga mavazi yasiyo na heshima imeendelea kushika kasi na kusambaa katika baadhi ya vyuo ambapo kwa mara nyingine tena imejitokeza wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ).

Waanzilishi wa kampeni hiyo ni Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na siku chache zilizofuatia Chuo Kikuu cha Tumaini, Kampasi ya Dar es Salaam ilipanga kutoa rasmi mwongozi kuhusiana na jambo hilo.

Katika mahafali hayo ya 15 ya MSJ, wanafunzi wa chuo hicho kikongwe cha binafsi, nao wamelaani vikali tabia ya uvaaji wa mavazi hayo kupitia ushairi wao waliousoma wakati wa hafla hiyo.

Wanafunzi wa chuo hicho walipobainisha hayo wakighani shairi kwenye mahafali hayo yaliyofanyika Machi 31, mwaka huu katika Ukumbi wa JKT Nane Nane mjini hapa.

Wakisoma shairi hilo mbele ya mgeni rasmi Katibu wa Baraza la Habari Tanzania ( MCT) Kajubi Mkajanga na viongozi wengine kwenye mahafali hayo, waghani wa shairi hilo pamoja na kuzungumzia mambo mengine, ubeti wa nane ulilaani nguo fupi zinazovaliwa mwilini na baadhi ya wasichana wakiwemo wanafunzi wenzao.

Pamoja na kulaani uvaaji wa nguo fupi na vimini, wanafunzi wa chuo hicho walitumia fursa hiyo kuwaasa wahitimu wa mahafali hayo na watu wengine wachukue tahadhari juu ya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna kinga wala dawa na haujali rika.

Jumla ya wahitimu 139 wa fani ya uandishi wa habari ngazi ya cheti na diploma, pamoja na walimu wa shule za awali walitunukiwa na mgeni rasmi.

Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Said Dogoli alisema tangu kianzishwe miaka 17 iliyopita wahitimu 716 wa masomo ya Uandishi wa Habari wamesoma chuoni hapo na wengi wamepata ajira katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya Serikali na sekta binafsi.

SERA YA MAVAZI KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA DAR ES SALAAM (CBE) YAANZA KUTUMIKA RASMI, WATAKAOKIUKA KUKUMBANA NA ADHABU.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
28/3/2012, Dar es salaam.

Kaimu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Bw. Athman Ally Ahmed akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kutumika kwa sera ya mavazi chuoni hapo yenye lengo kupiga vita mavazi yasiyo ya heshima kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi wa kike na wale wa kiume wawapo chuoni.

Uongozi wa Chuo cha elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam umesema kuwa hautasita kumchukulia hatua mwanafunzi au mfanyakazi  yeyote atakayefika chuoni hapo akiwa amevaa mavazi yasiyo ya heshima huku ukitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kampeni hiyo yenye manufaa katika kujenga taifa lenye maadili mazuri.
Akizugumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Kaimu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Bw. Athman Ally Ahmed amesema chuo hicho kimefikia uamuzi huo kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi  wa kike na wale wa kiume wawapo chuoni hapo hali inayosababisha udhalilishaji wa utu wa wanafunzi ndani na nje ya chuo.
Amesema wanafunzi ambao wengi wao ni vijana chuoni hapo wamekuwa mstari wa mbele katika kuiga kila aina ya vazi kutoka tamaduni za watu wa magharibi hali ambayo ameielezea kuwa ni ukiukaji wa mila , desturi na tamaduni za mtanzania .
“Mtindo huu wa kuiga tamaduni za magharibi pasipokuangalia wapi tunakwenda haukubaliki hata kidogo,ukiangalia katika vyuo vingi vya elimu hapa nchini wanafunzi wamekuwa wakivaa mavazi ya ajabu na yasiyofaa kabisa katika maeneo ya chuo” amesema.
Amesema kuwa Chuo hicho  kimekaa na kubuni sera  ili kuyaondoa mavazi ambayo hayaruhusiwi kuvaliwa katika maeneo ya chuo  na kubuni sera ya mavazi kwa ajili ya wanafunzi  hali itakayowajengea  nidhamu wasomi  hao  wa fani mbalimbali pindi watakapomaliza masomo yao chuoni hapo.
Amefafanua kuwa  adhabu mbalimbali zitatolewa kwa wanafunzi watakaokiuka agizo la uvaaji wa mavazi yenye heshima amabazo ni pamoja na kuzuiliwa kupita getini kwa mwanafunzi husika kuingia katika eneo la chuo kwa wale wanaotoka nje ya hosteli na wale wanaoishi ndani ya eneo la chuo hawatapewa huduma yoyote kama vile kuingia darasani,kantini , maktaba au ofisi yoyote ya chuo.
Aidha amefafanua kuwa wanafunzi  ambao  hawatakua  tayari kufuata utaratibu huo watafikishwa mbele ya kamati ya nidhamu huku akibainisha kuwa adhabu itakayotolewa ni mwanafunzi kusimamishwa  chuo kwa  muda wa miezi mitatu.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo Bi. Bertha Kipillimba amesisitiza kuwa zoezi hilo litawahusu wafanyakazi wote wa kampasi ya Dar es salaam na wanafunzi  zaidi ya 6000 wa chuo hicho.
Amesema hivi sasa taratibu hizo za uvaaji wa mavazi yenye staha zimeingizwa kwenye kanuni za chuo  na kuongezwa kwenye masharti ya fomu za kujiunga na chuo hicho huku akifafanua kuwa tayari wametoa kipindi cha wiki mbili kwa utekelezwaji wa kanuni hizo na watakaokiuka kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni hizo.
Naye mlezi wa wanafunzi wa hicho (Dean of Students) Bw. Faustin China amefafanua kuwa umefika wakati wa wanafunzi hao kujitambua huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakinyoshewa vidole na jamii kuhusu suala la uvaaji na mienendo ya wanafunzi chuoni hapo.
“Tumesemwa vibaya kwa muda mrefu hatuwezi kuachia suala hili likaendelea, tunataka wanafunzi wetu wavae vizuri kwa mujibu wa kanuni tulizojiwekea ili kujenga heshima ya chuo” amesema.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uanzishawaji wa sera ya mavazi chuoni hapo wakieleza kuwa inaingilia uhuru wao wa kuamua huku wengine wakiupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuliona suala hilo na kulichukulia hatua ili kuleta na kulinda heshima ya chuo hicho.

Eneo la mbele la Jengo la Utawala la Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam. Chuo hicho kimeanzisha sera ya mavazi kwa wanafunzi wawapo chuoni hapo ambayo imeanza kutumika rasmi kwa kuwataka kuvaa mavazi ya heshima na wale wanaokaidi kuchuliwa hatua za kinidhamu.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO